The House of Favourite Newspapers

Mayele: Nitaifungia Yanga Mabao 20

0

TAYARI ameshaweka kimiani mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara, huyu ni Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ambaye ameliambia Championi Jumatano kuwa, msimu huu amepanga kuifungia timu hiyo zaidi ya mabao 20.


Mayele tangu atue ndani
ya Yanga mpaka sasa katika michezo minne ya ligi kuu ambayo amecheza kabla ya
mchezo wa jana dhidi ya Ruvu
Shooting amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao mawili.

 

Mabao hayo mawili alifanikiwa kuyafunga katika michezo miwili ya mwisho dhidi ya KMC na Azam FC, huku
akishindwa kutupia mbele ya
Kagera Sugar na Geita Gold.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele aliweka wazi matamanio yake ya kufunga mabao 20 msimu huu akiwa na Yanga ambayo anaamini mabao hayo yatatosha kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa msimu huu huku pia akisema kuwa anataka kufunika idadi ya mabao ambayo aliyafunga msimu uliopita katika ligi ya DR Congo.

 

“Natamani kufunga mabao kuanzia 20 na kuendelea msimu huu nikiwa na Yanga, idadi hiyo ya mabao naamini
itaisaidia Yanga kufanya
vizuri ikiwa pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ambayo ni malengo ya timu.

 

“Najua na wachezaji wengine watafunga mabao ya kutosha hivyo naamini yatasaidia timu kufanya vizuri lakini pia nahitaji kufunga mabao mengi kuzidi yale niliyoyafunga msimu uliopita nikiwa DR Congo ambapo
nilifunga mabao 13,” alisema
mshambuliaji huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply