The House of Favourite Newspapers

Mayweather: Nitamchakaza Vibaya Mpinzani Wangu

0

TAMBO! Huku siku zikiendelea kukatika kama kawaida mwanamasumbwi mwenye mbwembwe za pesa, Floyd Mayweather ameanza kutamba kwamba iwe isiwe ni lazima amshinde vibaya mpinzani wake, Conor McGregor katika pambano lao litakalofanyika Agosti 26, Las Vegas, Nevada nchini Marekani.

Mayweather ameyasema hayo baada ya kufanya mazoezi kwa saa nne mfululizo katika gym ya Ten Goose huku akiwa na kundi lake la TMT akiwemo staa wa NBA, DeMar DeRozan.

“Naweza kuteseka, kufanya mazoezi ya kufa mtu, wakati mwingine mpaka kubadilika rangi lakini mwisho wa siku nipate kile ninachokitaka ulingoni. Nitamchakaza sana mpinzani wangu siku hiyo,” alisema Mayweather kwa mbwembwe.

Na: Nyemo Chilongani

Leave A Reply