The House of Favourite Newspapers

Mazishi ya Mama Abdul, Ibada ya Kuaga Mwili Kanisani – VIDEO

Ni Ibada maalum ya kuuaga mwili wa Muigizaji mkongwe, Salome Nonge maarufu kwa jina la Mama Abdul, inafanyika katika kanisa la Romani Katoliki Mburahati.

Baada ya ibada hiyo mwili huo utatolewa na kuelekea katika makaburi ya Chang’ombe Maduka Mawili jijini Dar, leo Januari 28, 2019 kwa ajili ya mazishi.

Mama Abdul alifariki dunia juzi Januari 25, akiwa nyumbani kwake na inasemekana kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la homa ya ini.

Kabla ya Umauti kumfika Mama Abdul alikuwa akiigiza tamhiliya ya ‘Mwantumu’ inayorushwa na DSTV ambayo ndani yake ameshirikiana na Joti, lakini pia aliwahi kunga’ra kwenye filamu kama Kantangaze.

Comments are closed.