The House of Favourite Newspapers

Mbatia: Mnasubiri Maafa Yatokee, ‘Mnapiga Ramli Maisha ya Watanzania” – Video

MBUNGE wa Vunjo na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR Mageuzi, James Mbatia ameilalamikia Serikali akidai imeshindwa kuweka chombo maalum kwa ajili ya kukabiliana na maafa/majanga makubwa ya kitaifa yanapotokea.

 

Mbatia ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini dar es Salaam alipokuwa akizungumzaia kuhusu tkio la kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere Ziwa Victoria ambapo mpaka sasa takribani watu 100 wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 37 wakijeruhiwa.

 

“Serikali haikumpa majibu mwakilishi wa wananchi wa Ukerewe (Joseph Mkundi) alipozungumzia suala la hitirafu ya kivuko hicho, haya mambo ya maafa si ya kiitikadi, kila mtu ana wajibu wa kutoa mchango wake…. Mnasubiri mpaka maafa yatokee…. baada ya hapo kila kitu kinasahaulika…. mnapiga ramli maisha ya Watazania? Hatuhitaji tusubiri hadi maafa yatokee tuombe rambirambi,” amesema Mbatia.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.