The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji azuia usajili wa Ndemla Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amepanga kuwaboreshea mikataba baadhi ya wachezaji wake wazawa kwa sharti awe amecheza nusu ya mechi za Ligi Kuu Bara na michuano mingine waliyoshiriki.

 

Kati ya wachezaji waliopendekezwa kuboreshewa mikataba yao ni viungo wa timu hiyo, Said Ndemla na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ ambao wote hivi karibuni walikuwa wanatajwa kuwaniwa vikali na Yanga.

 

Ndemla yeye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku Mo akibakisha mwaka mmoja ambaye alikuwa anatajwa kutolewa kwa mkopo. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo amefi kia hatua ya kuboresha mikataba ya wachezaji hao kutokana na kutovutiwa na viwango vya wachezaji wazawa.

Mtoa taarifa huyo alisema, kama kungekuwepo na wachezaji wazawa wenye uwezo kushinda alionao hivi sasa, basi angefanya usajili hivyo amependekeza kuendelea na wachezaji hao katika msimu ujao.

 

“Ukiangalia viwango vya wachezaji wazawa waliopo kwenye timu nyingine hakuna waliowazidi waliopo Simba, hiyo ndiyo sababu kubwa inayomfanya kocha apendekeze kubaki nao na waboreshewe mikataba kwa wale ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu.

“Kocha anataka mchezaji mpya atakayesajiliwa Simba awe na uwezo mkubwa utakaompa changamoto mchezaji atakayemkuta siyo asajiliwe halafu akae benchi,” alisema sosi huyo.

 

Alipotafutwa Aussems alisema: “Tangu msimu huu wa ligi umeanza sijaona mchezaji mzawa aliyenivutia nimsajili. Nimependekeza kwa uongozi kuwaboreshea baadhi ya wachezaji mikataba yao kwa wale ambao inamalizika mwishoni mwa msimu.”

Tambwe Afunguka kurogwa na Donald Ngoma

Comments are closed.