The House of Favourite Newspapers

Mbelgiji Simba Aipa Siri Stars

KOCHA wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amesema kuwa mechi ya Tanzania na Lesotho ndiyo itakayoamua hatma ya Taifa Stars kushiriki Afcon mwakani.

Mwezi ujao Stars inavaana na Lesotho katika mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali kuchezwa hapa Tanzania. Timu hiyo ipo katika kundi L ambalo linaongozwa na Uganda.

Stars kwa sasa inanolewa na kocha Emmanuel Amunike ambaye ni raia wa Nigeria na mchezo uliopita timu hiyo ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Cape Verde Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra kocha huyo alisema; “Safari ya Tanzania kwenda Cameroon mwakani itaamuliwa na Lesotho ingawa ninaamini uwezo wa kocha Amunike pamoja na wachezaji wake kama wakipambana kwa bidii zote hii ndiyo itakuwa ndiyo tiketi yao wa kusonga mbele lakini ni lazima washinde mchezo huo.”

“Amunike ana timu nzuri na mimi sitaki kumuingilia sana kwenye kazi yake zaidi aendelee kupambana kwa ajili ya kuiona timu yake inafuzu na mimi nitafurahi kuona hivyo sababu Tanzania ni nchi nzuri na mimi nipo hapa nafanya kazi na kwenye timu hiyo pia kuna wachezaji wangu,” alisema Patrick.

Comments are closed.