The House of Favourite Newspapers

Mbeya City Waitaka Nafasi ya Azam, Waapa Kupambana Kufa na Kupona

0
              Timu ya Mbeya City imedhamiria kushika nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Azam FC kwa sasa

OFISA Habari wa Mbeya City Shaha Mjanja, amesema mipango yao kwa sasa ni kuwa katika nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara inashikiliwa na Azam FC yenye alama 28, Mbeya City ni ya tano ikiwa na alama 25 baada ya mechi 19.

                                Kikosi cha Mbeya City chenye maskani yake jijini Mbeya

Mjanja amesema: “Kwa sasa mikakati yetu ni kuwa katika nafasi tatu za juu na si vinginevyo japokuwa tupo nafasi ya tano lakini bado tuna mpango wa kupanda juu kutoka hapa tulipo.

“Japokuwa msimu ni mgumu hasa raundi ya pili timu zinapambania mafanikio yao, hivyo lazima tupambane kufika kwenye nafasi tunayoitaka.”

Timu hiyo ambayo imepoteza mechi nne za Ligi Kuu Bara msimu huu, imebakiwa na mechi 11 kumaliza msimu huu.

Leave A Reply