The House of Favourite Newspapers

Mbosso: Nina Muda Mrefu Sijawasiliana na Aslay

0

MKALI wa Bongo Fleva mwenye kupendelea mahadhi ya pwani, Mbosso amefunguka kuhusu uhusiano wake na wasanii waliokuwa wenzake kunako yamoto band hasa aslay. Mbosso anasema kwamba, kwamba bado huwa anawasiliana mara kwa mara na Enock Bella pamoja na Beka Flavour.

Hata hivyo, Mbosso anathibitisha kutofautiana kwake na Aslay huku akiweka wazi kwamba hawajawasiliana naye kwa kipindi kirefu. “Huwa tunazungumza zaidi na Enock Bella, Beka Flavour nawasiliana naye, aslay nina muda mrefu kidogo hatujawasiliana ila tunawasiliana. nikisema hatuwasiliani ni uongo, ila tunawasiliana tu,” anasema Mbosso.

Mbosso anasema kuwa, alipokuwa anatayarisha albam yake alifanya jitihada za kuwatafuta wanabendi wenzake wa zamani ili wafanye muziki pamoja na akafanikiwa kuwapata Enock na Beka. Anasema juhudi zake za kumpata Aslay ziligonga mwamba kwani alishindwa kuafikiana na mameneja wake ambao alikuwa anawasiliana nao.

“Kipindi naandaa albam yangu nilimcheki Enock, nikamcheki Beka, nikamcheki aslay kupitia uongozi wake. kwa wawili iliwezekana, kumpata Enock na Beka iliwezekana ila kwa upande wa uongozi wa aslay kidogo kulikuwa na uzito. Sikuweza kuilazimisha sana kwa sababu nafahamu hii ni biashara na kila mtu ana mikataba yake.

“Nilikuwa nawasiliana na meneja wake anaitwa chambuso ambaye pia alikuwa meneja wetu, Yamoto Band. aliniambia kwa wakati huo jambo hilo lilikuwa ngumu. nilimwambia sawa kama haiwezekani hamna tatizo, ila kwa sababu niko katika kupangilia uzinduzi nitawapa mwaliko.

Niliwaomba waje kwenye uzinduzi. waliitikia kuja kwenye uzinduzi, lakini nilishindwa kuufanya kwa sababu tulipatwa na msiba mkubwa sana. Tulipokuwa tunakaribia kufanya uzinduzi ndipo aliyekuwa rais wetu mheshimiwa magufuli akawa amefariki dunia hivyo sikuweza kufanya kitu,” anasema Mbosso.

Mbosso anasema hangeweza kuendelea kufanya wimbo na wanabendi wenzake wa kitambo kama alivyotaka kwani lengo lake lilikuwa afanye na wote watatu pamoja.

 

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply