The House of Favourite Newspapers

Wolper: Mume Wangu Sio Chawa

0

MWANAMAMA wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper anasema kuwa, kitendo cha yeye na mumewe, Rich Mitindo kusapoti biashara za watu wengine siyo kwamba wao ni chawa.

Anasema kuwa, umekuwa ni utamaduni wake hata kama mtu amemkosea, basi atamsamehe na kuendelea kumsapoti kwani hayo ndiyo maisha.

“Kumsapoti mtu siyo kwamba mimi ni chawa, wala mume wangu si chawa, ni utamaduni tuliojiwekea wa kusapotiana sisi kwa sisi na mtu mwingine yeyote ili tusonge mbele.

Hata kama mtu amenikosea ni jukumu langu kumsamehe na kuendelea kumuunga mkono kwa kile anachokifanya na hayo ndiyo maisha,” anasema Wolper au Mama P.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply