The House of Favourite Newspapers

Mbowe Atoka Karantini, Atinga Bungeni na “Corona” – Video

0

Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema #CoronaVirus ni janga ambalo linapaswa kupewa uzito kama ambavyo mataifa mengine yanafanya.

 

Amesema japokuwa Serikali imetoa tahadhari mbalimbali, bado kuna uzembe. Ameshauri kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Taifa ambacho kitasimamia masuala yote ya #Covid19 na kutoa wito kwa Serikali kushirikisha wadau wengine.

 

Ameeleza kuwa kuna umuhimu wa Kikosi hicho kushirikisha wanazuoni, madaktari, hospitali binafsi na taasisi mbalimbali ili janga hili lipewe uzito wa Kitaifa na lisibaki kwa Serikali peke yake.

 

Katika maelezo yake, Mbowe amesema tayari #CoronaVirus imeshaathiri uchumi wa nchi na alitegemea Bajeti ya Serikali ingekuja na mpango maalum na kutoa taarifa kuhusu athari hizo Bungeni, lakini mpaka sasa mipango ya Serikali ipo pale pale.

 

Kuhusu Uchaguzi, Mbowe amesema wamekuwa wakidai maridhiano ya nchi na #TumeHuru kwasababu wanaamini kwamba ili nchi iweze kupata maendeleo, ni lazima kuwe na viongozi wanaopatikana kwa misingi ya Demokrasia.

 

Amesema Kifungu no. 74 na 75 cha Katiba kinahitaji marekebisho machache na endapo upande wa Serikali utaonesha ushirikiano, maridhiano yatakuwepo na Uchaguzi utakuwa wa haki.

 

 

Leave A Reply