The House of Favourite Newspapers

Slay Queens Walivyojiongeza

0

CHANGAMOTO katika maisha hutokea ili uwe na kitu cha kujifunza, ndio maana kuna msemo usemao kwamba, ‘majaribu ni sehemu ya kipimo’, kwa maana ya kwamba kuna muda lazima binadamu tupitie kwenye majaribu ili yatufunze jinsi ya kukabiliana na changamoto katika maisha.

 

Na siku zote mtegemea cha ndugu hufa masikini, ikiwa leo hii mtu huwezi kupambana au kusimama mwenyewe kwa kutegemea pesa zilizo mfukoni mwa mtu basi muda si mrefu utapotea.

 

Hii tabia imekuwa kwa akina dada wengi wa mjini wenyewe hupenda kujiita slay queens, wao hupenda kuishi maisha wanayoyajua wao, mara nyingi akiwa na shida na kitu f’lani basi simu moja ameshapata anachokitaka, mwisho wa siku akipatwa na matatizo anakuwa mwenyewe na familia yake, wale watu aliokuwa akiwategemea kwa kuwaburudisha kisha apate pesa wanakuwa hawapo tena karibu yake.

 

Miaka michache iliyopita hali hii ilikuwa kwa kiasi kikubwa hasa kwa mastaa wetu wa kike hapa Bongo, wengi wao walionekana wakiishi maisha ya kifahari sana na kutembelea ndinga kali huku kazi wanazofanya zikiwa hazisadiki kabisa bata kubwa wanazofanya.

 

TUNDA

Huyu ni video vixen maarufu hapa Bongo, jina lake halisi anaitwa Annastazia Kimaro, ila hupenda kujiita Tunda kwa sababu ndio jina linalomsaidia kupata ugali, miaka michache iliyopita alionekana ndio staa anayeongoza kwa kula sana bata ndani na nje ya nchi, asilimia kubwa ya maisha yake ilikuwa ni kuishi hotelini.

 

Hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki zake kumtungia jina na kuanza kumuita ‘Tunda mahoteli’ baadhi ya watu hawakufurahishwa na aina ya maisha anayoishi kwani pesa alizokuwa akitumia kuspendi na kazi anayoifanya ni vitu viwili tofauti.

 

Lakini hivi karibuni ameonekana kubadilika kutoka kuitwa Tunda mahoteli mpaka Tunda mjasiriamali, ambapo wiki iliyopita amefungua duka lake la nguo alilolipa jina la Tunda Boutique lililopo Kinondoni jijini Dar.

 

NAI

Naye ni video vixen maarufu Bongo, jina alilopewa na wazazi wake ni Nairath Ramadhani, ni miongoni mwa wasichana ambao awali walipenda sana kujirusha katika viwanja mbalimbali huku kazi anayofanya ikiwa haimshawishi mtu kuamini kuwa ndio anapata pesa yakufanya mambo yote hayo.

 

Siku zilivyozidi kwenda mrem-bo huyu naye aliamka kutoka usingizini, akapunguza kidogo mambo ya uslay queen na sasa anamiliki salon yake mwenyewe inayodili na mambo ya make up kwa wanawake pamoja na kuten-geneza nywele wa-naume.

 

LYYN

Jina lake halisi anaitwa Irene Louis, ila mwenyewe hupenda kujiita Lyyn kutokana na kazi anazofanya, naye hatofautiani sana na Tunda kwani amekuwa akiandamwa na mashabiki huko mtandaoni kuwa anaendekeza starehe kuliko kujali maisha yake na kufanya mambo ya maana.

 

Hivi karibuni baada ya hali kuwa mbaya mrembo huyu naye aliamua kuachana na mambo ya kuwa slay queen na kuamua kuanza kufanya kazi ya kuimba muziki ambapo kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Maneno.

 

IRENE UWOYA

Ni miongoni mwa mastaa walioandamwa na skendo za kula bata na kumwaga hovyo pesa hadharani, huku kazi ya usanii tu anayoifanya ikiwa haiwaridhishi watu wengi wanaopenda kufuatilia maisha yake.

 

Naye baadae aliamua kufungua baa maeneo ya Sinza aliyoipa jina la Last Minutes ili iwe inamuingizia kipato lakini hakuishia hapo kwani hivi karibuni pia amezindua reality show yake aliyoipa jina la I’am Every Woman ambayo inarushwa katika televisheni moja maarufu hapa mjini.

 

 

GIGY MONEY

Kama ukiambiwa utaje listi ya mastaa wa kike Bongo, nina imani kwamba hautasahau kutaja jina la mwanamama huyu kutokana na skendo nyingi anazokuwa nazo mtandaoni.Anaitwa Gift Stanford, ila mwenyewe hupenda kujiita Gigy Money, ni miongoni mwa slay queens mjini ambao walikuwa wanapenda kuishi kwa kutegemea pesa ambazo hawajazitolea jasho lao.

 

Lakini baada ya hali kuzidi kuwa mbaya huku wale waliokuwa wakiwategemea kuwapatia pesa nao wakitokomea kusikojulikana, hivi ka-ribuni ameonekana kubadilika na kuhamishia up-epo sehemu nyingine, ambapo mbali na kazi ya muziki anay-ofanya sasa hivi ni balozi wa taulo za kike ambazo humuin-gizia kipato cha kujikimu yeye na familia yake.

MAKALA: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply