The House of Favourite Newspapers

Mbowe na Wenzake Wafikishwa Mahakamani – Video

0

MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake, leo Jumatatu, Septemba 6, 2021 wamefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, iliyopo Mawasiliano Dar es Salaam, kwa ajili ya kusikiliza hatma ya mapingamizi yao dhidi ya hati ya mashtaka yanayowakabiri.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyounganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.

Watuhumiwa hao pia wanakabiliwa mashtaka mbalimbali ikiwemo;

1. Kula njama za kutenda ugaidi (kulipua vituo vya mafuta)
2. Kutenda ugaidi kwa kudhuru viongozi wa serikali ikiwemo kusababisha majeraha kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

3. Mbowe anadaiwa kutoa laki 6 kwa ajili ya kufadhili matendo ya Kigaidi.

4. Watuhumiwa wote kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi.

5. Mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi

6. Mshtakiwa wa kwanza akituhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 

 

Mbali na Freeman Mbowe, wanatuhumiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya.

 

Leave A Reply