The House of Favourite Newspapers

Mbowe: “Serikali Inaongozwa Kibabe”…. Majaliwa Amjibu – Video

0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema vyama vya siasa nchini havijazuiwa kufanya shughuli zake za kisiasa isipokuwa kumewekwa utaratibu wa vyama hivyo kufanya shughuli hizo kwenye maeneo yao ambayo wamepata ridhaa ya kuongoza. 
“Ni miaka minne sasa tangu serikali iweke zuio kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, na tunavyozungumza leo Mheshimiwa Waziri Mkuu ni siku 262 zimebaki kufika tarehe 25 Oktoba siku ambayo nchi yetu itafanya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa busara zako na za serikali ambayo wewe ni kiongozi mwandamizi unafikiri ni lini utaruhusu vyama vya siasa vifanye wajibu wake wa uenezi kwa mujibu wa sheria ili kujiandaa na uchaguzi mkuu, Serikali ina mpango gani wa kuwezesha taifa kupata tume huru ya uchaguzi ambayo itahakikisha kwamba uchaguzi huu unakuwa huru, wa haki na wa halali,” Freeman Mbowe.

Aidha, akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila tumeweka taratibu muhimu kwa wale viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao, ratiba za uchaguzi zitatolewa na kueleza lini shughuli za kampeni zitaanza.

“Kwanza nataka nikanushe Serikali haiongozi kibabe, Mbowe ni kiongozi tunazungumza na kubadilishana mawazo na lengo ni kulifanya taifa liwe salama, Watanzania wanahitaji maendeleo na hakuna Mbunge au Diwani aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yake.

 

“Tume ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa katiba na kwa mujibu wa katiba ya nchi kipengele 74 (7) (11) (12) inaeleza kwamba hiki ni chombo huru, kimeelezwa pia kwenye katiba pale, na chombo hiki hakipaswi kuingiliwa na chombo chochote, iwe rais wa nchi, iwe chama chochote cha kisiasa au mamlaka ya aina yoyote ile haipaswi kuingiliwa.

 

“Kama ni chombo huru kwa mujibu wa katiba ndiyo tume huru, sasa kunaweza kuwa na tofauti ya neno huru hili linatakiwa litambulike vipi, hiki chombo kipo kinafanya kazi yake, kinajitegemea bila kuingiliwa na mtu yeyote.

 

“Vyama vya siasa havijazuiwa kufanya shughuli zake ila tumeweka taratibu muhimu zinazowezesha vyama kufanya shughuli zake za kisiasa kama ambavyo tumekuwa na uhuru pia kwa wale wanasiasa wote walioomba ridhaa katika maeneo yao wakapata ridhaa hiyo kuendelea kufanya shughuli kwenye maeneo yao ambayo wamepata kibali kama vile madiwani na wabunge wanaendelea kufanya shughuli za siasa kwenye maeneo yao kama ambavyo wao wanapaswa kufanya shughuli hizo,” Kassim Majaliwa.

 

 

Leave A Reply