The House of Favourite Newspapers

Mbunge Taletale Awaombea Wahitimu Mgambo Nafasi 5 Kujiunga JKT Mkuyuni

0

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Bakari Msurwa amehitimisha mafunzo ya jeshi la akiba wilayani Morogoro. Hafla ya kilele cha mafunzo ya jeshi la akiba wilayani Morogoro imefanyika leo December 15, Mkuyuni na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Mh. Mbunge, viongozi mbalimbali wa wilaya pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Mhe. Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamis Shabani Taletale amewapongeza wahitimu wa mafunzo ya jeshi la Akiba kwa juhudi na nia ya uzalendo walio nayo, na Kuwatia moyo wahitimu wa jeshi la Akiba  kutokana na changamoto wanazokutana nazo wakati wa mafunzo, Pia ameweza kuwaombea na Kupata nafasi 5 kwa wahitimu wenye sifa na vigezo vya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mkuu wa Wilaya Mhe. Bakari Msurwa amempongeza Mhe. Mbunge kwa jitahada zake na uchapajikazi wake kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Morogo Kusini Mashariki na ameagiza vija hao 5 kuchaguliwa mapema ili waweze kujiunga na JKT.

Leave A Reply