The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Hafsa Mossi Auawa

0

amosozi

Hafsa Mossi.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi, Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura leo.

Bi. Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.

Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.

mossi

Msemaji wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.

“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.

Waziri wa Mambo ya Nje, Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.

“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo #Bujumbura ya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa #EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na #EAC,” Ameandika kwenye Twitter.

Chanzo: BBC

Leave A Reply