The House of Favourite Newspapers

Shilole: Nimejipanga kimataifa

0

shilole (1)MWANAMUZIKI wa Muziki wa Bongo Fleva, Shilole Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kusema kuwa amejipanga ipasavyo kuanzia kwenye mashairi hadi mpangilio wa muziki wake kuhakikisha anasonga mbele kimataifa zaidi.

Shilole ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Say My Name’ huku pia akisifika kwa umahiri mkubwa wa kulichezea jukwaa ameamua kuja kivingine.

Akizungumza na Mikito Jumatano, alisema kuwa, kutokana na soko la muziki kwa sasa kulipa ameona ni vyema akajipanga ili kuhakikisha anabadilika na kuendana na soko la nje kwa kutoa kazi zenye ubora wa kimataifa.

“Soko la muziki kwa sasa limekua na linalipa kulinganisha na huko nyuma na kwa upande wangu nimeamua kujipanga zaidi ili kuwa bora kuanzia kwenye mashairi na hata uchezaji ikiwa ni pamoja na upande wa kujifunza zaidi Lugha ya Kiingereza,” alisema Shilole.

Leave A Reply