The House of Favourite Newspapers

Mbwa Atunukiwa Tuzo ya Heshima ya Rais kwa Kugundua Mabomu Ukraine

0

Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky amemtunukia tuzo ya heshima ya Rais mbwa aliyepewa jina Pattern kwa huduma zake tangu uvamivi wa Urusi.

 

Mbwa huyo mwenye umri wa miaka miwili na nusu amekuwa shujaa wa kitaifa nchini Ukraine, ishara ya upinzani wa Ukraine dhidi ya Urusi. Mbali na kubaini marundo zaidi ya 200 ya nyaya zinazohusishwa na vipulizi, mwezi April alitajwa kugundua mabomu zaidi ya 90.

 

“Ninataka kuwatunuku mashujaa hawa wa Kiukreni ambao tayari wanasafisha ardhi yetu.”Rais Zelensky alisema katika hafla ya Jumapili huko Kyiv kwamba mbwa huyo sio tu anasaidia kubaini vilipuzi, lakini pia hufundisha watoto wetu kanuni muhimu za usalama katika maeneo ambayo kuna hatari.

 

Sherehe ya tuzo hiyo pia ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, ambaye aliwasili Ukraine siku ya Jumapili. Justin Trudeau alitangaza kwamba Canada itatoa silaha zaidi na vifaa kwa Ukraine.

 

Rais Zelensky alikabidhi medali kwa mbwa huyo na mmiliki wake My Hello Ilyo. Mbwa huyo mdogo kiumbo amekuwa maarfu nchini chini ya kitengo cha usalama tangu uvamizi wa Urusi.

Leave A Reply