The House of Favourite Newspapers

Msigwa: Mbowe Aliondolewa Walinzi – Video

0

MUDA mfupi baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kushambuliwa na watu wasiojulikana jijini Dodoma baadhi ya viongozi wa chama hicho na wadau mbalimbali wametoa maoni yao.

 

Akizungumza na chombo kimojawapo cha habari nchini, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amedai kuwa shambulizi hilo la kiongozi wao wa chama lina dalili za kisiasa.

 

“Waliokuwa wakimshambulia walikuwa wakiongea maneno ambayo yanaashiria kuwa walilenga kwenda  kumshambulia na shambulizi lake lina muelekeo wa kisiasa,” ameeleza Mnyika.

 

Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa ambaye ametangaza nia ya kuwania urais hivi karibuni amesema kuwa wakati Mbowe anashambuliwa hakuwa na walinzi wake.

 

“Wakati anapanda ngazi wakashuka watu watatu wakamuambia wewe unaisumbua sana Serikali, sisi hatuna mpango wa kukuua ila tunataka tukuvunje ili ushindwe kufanya kampeni,” amesema Mchungaji Msigwa.

Msigwa ameeleza kuwa walinzi waliokuwa wakimlinda Mwenyekiti huyo waliondolewa kutokana na suala la tishio la ugonjwa wa corona.

 

Naye Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amelihusisha suala hilo na tukio la Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara (Tundu Lissu) kutangaza nia ya kuwania urais akidai kwamba waliomshambulia Mbowe wanampelekea ujumbe Lissu huku akitaka Mwenyekiti huyo wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani bungeni kupewa ulinzi.

 

“Kwa nini Mbowe halindwi? Kumlinda Mbowe ni kuilinda Katiba yetu na si kuisaliti CCM.  Katiba inataka tuwe na wapinzani na chama kikuu cha upinzani,” ameeleza Karume.

 

Leave A Reply