The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Bushiri Atoroka Sauz Baada ya Dhamana

0

MCHUNGAJI maarufu Barani Afrika, Bushiri na  mke wake Mary, wametoroka nchini Afrika Kusini na kurejea kwao Malawi baada ya kuachiwa jela kwa dhamana kufuatia kushtakiwa kwa utapeli na utakatishaji fedha.

 

Mchungaji Bushiri, ambaye alisema kuwa anataka kusafisha jina lake, amedai kulikuwa na majaribio kadhaa ya kutishia maisha yake na mamlaka ya Afrika Kusini haikutoa ulinzi wowote kwake na kwamba kukwepa dhamana ni njia ya busara ya kulinda maisha yake.

 

Ametorokaje nchini Afrika Kusini?

Kuna madai kuwa Mch. Bushiri alitoroka na ndege ya Rais wa Malawi akiwa na Rais Lazarus Chakwera, lakini Ofisi ya Rais wa Malawi imekanusha kuhusika.

 

Waziri wa sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema serikali haitasita kumfuatilia, kumkamata na kumrejesha Afrika Kusini asikilize kesi yake lakini wakati huohuo Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Eisenhower Mkaka, amesema ni jukumu la serikali kulinda raia wa Malawi lakini na kuongeza kuwa Rais Chakwera ni mtetezi wa sheria na mianya yote ya kidiplomasia itabaki wazi.

 

Mchungaji Bushiri ni nani?

Ni mchungaji milionea ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa miongoni mwa wachungaj tajiri zaidi barani Afrika, na alitajwa kuwa na matukio tata ambapo aliwahi kudai   aliwaponya watu wenye  virusi vya ukimwi, alifanya vipofu waone, na kuna madai aliwahi kuonekana akitembea angani.

 

Amekulia katika Kijiji cha Mzuzu, Malaw,i na kuhamia Pretoria Afrika Kusini ambako ndiko kulikuwa na Kanisa lake – ‘The Enlightened Christian Gathering’.   Alipata umaarufu kwa kujaza umati wa watu kwenye mahubiri yake kwenye viwanja vya mpira.

 

Mchungaji huyu anashutumiwa nini?

Mch. Bushiri anashutumiwa kufanya utakatishaji fedha, utapeli na kufanya matukio ya uhalifu akiwa yeye na mkewe na watu wengine watatu. Kesi yake inajumuisha mamilioni ya dola.

 

Kesi ilikuwa imefikia wapi?

Mchungaji alifikishwa mahakamani Oktoba 21, 2020, kusikiliza kesi zake na kupewa dhamana mwezi Novemba. Kesi yake ilipangwa kuanza kusikilzwa mwezi Mei mwakani.

 

Leave A Reply