The House of Favourite Newspapers

Watanzania Waaswa Kudumisha Amani na Upendo Mfungo wa Ramadhan

0

Watanzania waumini wa dini ya Kiislamu nchini kote wamehimizwa kudumisha amani na upendo miongoni mwao wakiwa wanaendelea na mfungo wa Ramadhan.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah wakati walipokutana na wateja, washirika, na wadau wao mbalimbali wakati walipoandaa futari ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

“Mwezi wa Ramadhan ni kipindi muhimu kwa waumini wa dini ya Kiislamu na nguzo muhimu ambapo huwasogeza karibu kupitia mfungo unaosindikizwa na ibada. Tuitumie fursa hii kuendelea kujizatiti kwetu katika maendeleo na ustawi wa jamii zetu nchini na taifa lote kwa ujumla,” alielezea Bi. Abdallah.

Akizungumzia umuhimu wa kufunga na kujumuika kwa pamoja wakati wa Ramadhan, Bi. Abdallah amesisitiza namna watu wanavyoweza kufanyika huku wakihamasisha kuwa na mazingira endelevu pamoja na afya bora.

“Serikali ya Tanzania inafanya jitihada za makusudi katika kuhamasisha matumizi ya gesi asilia ya kupikia, na Puma Energy tunajivunia kuunga mkono juhudi hizi. Kwa kuhamia katika matumizi ya gesi asili kama suluhisho la kupikia, jamii za Kitanzania zinaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa na kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kuongezea, gesi safi asilia ya kupikia pia hupunguza uhachuzi wa hewa majumbani, hivyo kuboresha afya na ustawi wa watu na familia,” aliongezea.

Akisisitiza katika malengo ambayo huwakutanisha kwa pamoja Waislamu wote nchini wakati wa mfungo wa Ramadhan, kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Zaira Mkologoye ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, amebainisha kuwa mwezi mtukufu ni fursa ya kuimarisha upendo na mshikamano sio tu kwa waumini pekee bali na jamii nzima kwa ujumla.

“Kwa ajili ya mwezi huu mtukufu, ninawaomba tujitahidi kuyafuata mafundisho ya Uislamu kwa kuonyesha upendo na matendo ya huruma. Tuwasaidie wale wenye uhitaji, na kudumisha umoja miongoni mwa jamii yetu. Kwa kufanya matendo memo na ya ukarimu, sio tu kwamba tunatimiza wajibu wetu wa kiimanini bali pia tunachangia jamii yenye mshikamano na kujali zaidi. Ningependa kuwapongeza Puma Energy Tanzania kwa shughuli zao za kijamii, na ninawaasa muendelee na miradi hii ili kuzinufaisha jamii zenye uhitaji zaidi,” alimalizia Sheikh Walid Alhad Omar.

Akishukuru, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dk. Selemani Majige ametoa shukrani zake za dhati kwa mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuungana na kampuni ya Puma Energy Tanzania na wadau wake kushiriki shughuli hii muhimu ya Iftar, akasisitiza kuendeleza ushirikiano wa kibiashara unao ifanya kampuni ya Puma Energy Tanzania iendelee kufanya vizuri sokoni huku aki ahidi jitihada zaidi katika kuboresha huduma zetu ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu na gawio stahiki kwa wanahisa. Mwenyekiti alimalizia kwa kuwatakia wakristo wote heri ya sikuu ya pasaka.

Tukio hili lilihudhuriwa na washirika, wadau, na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya usambazaji wa mafuta na nishati nchini. Pia, ilitoa fursa ya kipekee ya kukutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kuhudumia jamii ya Watanzania.

Miongoni mwa jitihada za Puma Energy Tanzania ni kupitia mradi wa kuwezesha shule za msingi za umma ambao unaunga mkono programu ya WASH inayolenga kuboresha mahudhurio ya wanafunzi, kuendelea na masomo, na kuwa na matokeo bora ya elimu. Pia imekuwa na mkakati endelevu wa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi nchi nzima.

 

Leave A Reply