The House of Favourite Newspapers

Messi, Antonella Kufunga Ndoa Leo Hii

0

LABDA ulikuwa unasikilizia kwa makini sana kujua ni lini staa wa Argentina na FC Barcelona atafunga ndoa na mama watoto wake, nikutonye tu kwamba staa huyo na mzazi mwenzake, Antonella wanafunga ndoa leo hii huku ikiwa ni mchana kwa huko Argentina.

Mastaa mbalimbali wameahidi kuhudhuria harusi hiyo na kwa kifupi tu ni kwamba tayari yule mwanamama mwenye mvuto mkubwa, mwanamuziki na mke wa Gerard Pique amekwishawasilia nchini humo kwa ndege ya kukodi akiwa na mume wake.

Mbali na hao, pia mastaa kibao wakiwemo Luis Suarez, Neymar, Xavi, Cesc Fabregas na Carlos Puyol watakuwemo kwenye harusi hiyo itakayofungwa mbele ya umati wa watu.

Na Nyemo Chilongani, (GPL)

 

Leave A Reply