The House of Favourite Newspapers

MEYA WA DAR AACHIWA DHAMANA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita baada ya kumshikilia kwa zaidi ya saa 24.

 

Mwita ambaye ni diwani wa Vijibweni (Chadema) alikamatwa na polisi juzi Desemba 1, 2018 saa 11 jioni baada ya kumaliza kikao cha kutunisha mfuko wa vijana na kuachiwa jana saa 2 usiku akituhumiwa kufanya maandamano bila kuwa na kibali.

 

Wakili wa Meya huyo, Alex Massaba amesema baada ya polisi kuchukua maelezo walimuachia kwa dhamana na kumtaka aripoti leo kwa mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kigamboni.

ACT – “Mungu amuadhibu MAGUFULI, kamwe Hatuwezi kumuombea”

Comments are closed.