The House of Favourite Newspapers

Meza ya Wazalendo…. Maria Sarungi, Masha Kupamba Kongamano

0
Maria Sarungi.

WATOA mada mashuhuri nchini, Maria Sarungi Tsehai anatarajiwa kuungana na Lawrence Marsha, Eric Shigongo, Mzee Shaba na Benjamin Fernandes katika kongamano la kihistoria la Meza ya Wazalendo litakalofanyika Septemba 2, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Benjamin Fernandes.

Akizungumza na Risasi Vibes, mratibu wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya Vijana Wazalendo wa Kitanzania, Tanzania Youth Patriots (TYP), Vian Nchimbi alisema kuwa, siku hiyo ratiba itaanza rasmi saa 7 mchana hadi saa 11 jioni ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshu-ghulikia Muungano na Mazingira, January Makamba.

Lawrence Marsha.

“Tutakuwa pia na mtangazaji maarufu kutoka Kituo cha Redio cha Sauti ya Amerika (VoA), Shaka Ssali tunawa-omba wote mje kuwa sehemu ya mjadala mpana ambapo mambo mbalimbali juu ya Utanzania wetu na dhana nzima ya uzalendo kwa ujumla yatazung-umzwa.

Shaka Ssali.

“Wanafunzi wa sekondari, vyuo vya elimu ya juu, taasisi mbalimbali na wananchi wote mnakaribishwa kwani kiingilio ni bure kabisa,” alisema Vian.

Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu au ujumbe wa SMS au WhatsApp kupitia namba 0769984781. Kongamano hili limedhaminiwa na Clouds Media Group na Global Publishers.

MIMI NI MZALENDO, NITAHU-DHURIA, WEWE JE?

Makamba, Shaka, Shigongo, Sarungi, Marsha Kukutana Kwenye Meza ya Wazalendo


Leave A Reply