The House of Favourite Newspapers

Mfugale Kuzikwa Jumatatu Ifunda, Iringa

0

Mwili wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, aliyefariki dunia Juni 29, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma, unatarajiwa kuzikwa Jumatatu ya Julai 5, 2021 nyumbani kwao, Ifunda mkoani Iringa.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati ya mazishi, shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, zitaanza leo, Julai Mosi, 2021 ambapo mwili huo utaagwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kisha mwili utasafirishwa mpaka jijini Dar es Salaam ambako utaenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo.

 

Kesho Ijumaa, Julai 2, 2021 mwili huo utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambako waaombolezaji watapata fursa ya kutoa salamu za mwisho, kisha jioni, mwili huo utapelekwa nyumbani kwa marehemu, Kimara Temboni.

 

Jumamosi ya Julai 3, mwili huo utasafirishwa kuelekea Ifunda, Iringa ambako mazishi yatafanyika Jumatatu.

Leave A Reply