The House of Favourite Newspapers

Mfungwa Aliyesamehewa na JPM Aua, Naye Auawa – Video

0

Mtu mmoja ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John Magufuli, Desemba 9, mwaka huu, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania Bara, amedaiwa kuvamia na kuwachoma visu watu 6 huku mmoja wao akifariki dunia hapo hapo.

 

Tukio limetokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Mjini Bukoba Mkoani Kagera. Inadaiwa kuwa, baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia hadi kumuua.

 

Mmoja kati ya waliokuwa naye, amethibitisha kuwa alikuwa mfungwa ambaye naye aliachiwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Magufuli.

 

Aidha, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, ACP Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

MFUNGWA ALIYESAMEHEWA AMTOA UTUMBO MWENZIYE, AMUUA, NAYE AUAWA…!

Leave A Reply