The House of Favourite Newspapers

Mgahawa Dar wanusulika kuungua

0

1Mlango wa jengo hilo.

2 Moshi ukiwa umetanda ndani ya chumba cha mgahawa huo.

3Gari la jeshi la zimamoto likiwa eneo la tukio.

4Baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo wakishuhudia uokoaji.

5 Moja ya friji lililokuwemo ndani likitolewa.

6Likiwa limeungua.

7Kikosi cha zimamoto kikiwa kazini.

8 Mmiliki wa jengo hilo, Hussein Said akihojiwa na wanahabari juu ya chanzo cha moto huo

9Baadhi ya viti na meza vilivyokuwemo ndani ya mgahawa huo.

MGAHAWA mmoja uliopo ndani ya jengo la ghorofa sita lililopo mtaa wa Lumumba mkabala na Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, umenusurika kuungua baada ya kutokea hitilafu ya umeme iliyodaiwa chanzo chake ni waya wa friji ulioshika cheche za moto na kuwaka.

Akizungumza na mwanahabari wa mtandao huu, mmiliki wa jengo hilo, Hussein Said alisema hitilafu hiyo ilianzia katika chumba cha mgahawa kilichopo chini na hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya kuungua kwa baadhi ya viti na  vyombo.
Alisema kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio kwa muda muafaka na kuuzima moto huo usisambae wala kuleta athari nyingine yoyote

Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Reply