The House of Favourite Newspapers

Mgogoro Ukubwa wa Kaburi Wachelewesha Maziko

0

MAZISHI yalicheleweshwa kwa muda wa saa mbili baada ya mgogoro wa ukubwa wa kaburi ambamo atazikwa marehemu, kuibuka katika maziko ya mzee mwenye umri wa miaka 98 nchini Uingereza.

 

Mtoto wa marehemu, Peter Worby, alisema baba yake, William, alitakiwa kuzikwa lakini Padre kutoka kanisa la Old Hall Green huko Hertfordshire alisema kina cha kaburi hilo ni kifupi kuliko inavyostahili hivyo hawezi kuendesha ibada ya maziko hayo.

 

Baada ya kufikiwa kwa makubaliano, kasisi huyo aliruhusu mazishi ya mzee huyo kuendelea, lakini Worby alisema familia yake ilinyimwamuda wa kuomboleza.” Aidha, Askofu wa Kanisa Katoliki aliomba msamaha kwa kuwaongezea msongo wa mawazo.

 

Kwa mujibu wa chama kinachoshughulikia masuala ya waliokufa kilisema, hakuna kina maalum ambacho kimepitishwa kisheria lakini Wizara ya Sheria inapendekeza angalau kaburi liwe na kina cha sentimita 61 kuanzia kwenye mchanga wa jeneza linapoishia hadi eneo la juu ya ardhi.

 

Leave A Reply