The House of Favourite Newspapers

Mgombea: Nimetekwa na watu 105, nimebakwa!

0

UNYAMA! Zikiwa zimebaki siku 10 ili kupiga kura Oktoba 25, mwaka huu katika uchaguzi mkuu, mgombea wa Udiwani Viti Maalum wilayani Butiama, Mara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyetajwa kwa jina moja la Upendo (39), anadai kutekwa na kundi la vijana wapatao 105 kisha kubakwa na kuachwa katika hali mbaya.

ILIKUWA SAA 11:30 JIONI

Tukio hilo la kinyama na kikatili lilijiri Oktoba 7, mwaka huu, saa 11:30 jioni katika Kijiji cha Butuguri wilayani Butiama ambapo mgombea huyo alikumbwa na mkasa huo baada ya gari la mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama kupitia Chadema, Yusufu Khazi alilokuwa akisafiria kushambuliwa na kuvunjwa vioo na taa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lenye nambari za usajili T 973 AEV lililokuwa likiendeshwa na Masembo Paulo liliwabeba baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wakitokea kwenye mkutano wa kampeni za ubunge katika Kijiji cha Sirorisimba ambapo mgombea wao wa ubunge yeye aliondoka na helikopta ‘chopa’.

UVAMIZI

Ilidaiwa kwamba, gari hilo lilipofika Butuguri ndipo likavamiwa na vijana hao ambao walirusha mawe na kuvunja vioo, taa na kuwajeruhi watu tisa waliokuwa ndani ya gari hilo kabla ya kumfanyia unyama mgombea huyo.

AOKOTWA HOI

Ilielezwa kwamba, baada ya kumfanyia unyama huo, jamaa hao walimuacha akiwa hoi ndipo akaokotwa na wasamaria wema ambao walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa ajili ya matibabu.

Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo, Florah Tumaini Ryana, mgombea ubunge wa Viti Maalum katika jimbo hilo kupitia Chadema ambaye alikuwa ndani ya gari hilo na kunusurika baada ya kutoroka kwa kukimbia, alieleza kwamba, anahisi vijana hao waliandaliwa mahususi kwa ajili ya tukio hilo.

WALIOJERUHIWA WAFUNGULIWA MASHTAKA

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, inadaiwa kuwa majeruhi tisa walijikuta wakifunguliwa mashtaka na viongozi wa chama kimoja cha upinzani kuhusiana na tukio hilo hali iliyozua maswali miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Kesi hiyo yenye namba BUT/IR/830/2015 –SHAMBULIO ilifunguliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Butiama.

Katika jalada la kesi hiyo, watu hao tisa wanatuhumiwa kuvamia kambi hiyo wakiwa na mapanga kwa lengo la kuwawekea vijana hao sumu kwenye chakula.

POLISI WATHIBITISHA

Habari kutoka ndani ya kituo hicho cha polisi zilieleza kwamba, waliojeruhiwa na kufunguliwa mashtaka kituoni hapo ni John Simba Mzuzu (Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Butiama), Pendo Juma (Diwani Viti Maalum Kata ya Sirorisimba) na Yasinta Hassan (Diwani Viti Maalum Kata ya Kukirango).

Wengine ni Semi Jumanne (Mwanachama wa Chadema), Edson Kanza (Mwanachama wa Chadema), Sospeter Mruta (Katibu Baraza la Vijana wa Chadema Wilaya ya Butiama), Masemba Paulo na Siliakusi Rashid.

Kwa upande wao polisi wilayani Butiama walithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Butiama na kwamba wanaendelea na uchunguzi zaidi.

ASIMULIA MKASA MZIMA

Kwa upande wake mgombea huyo, akiwa na maumivu makali katika kituo hicho cha polisi, alilisimulia Amani mkasa mzima kwamba, alishangaa walipofika kijijini hapo kuona kundi la vijana hao waliokuwa na silaha za jadi waliwavamia kisha kuwateka na kuanza kuwashushia kipigo.

“Walikuwa vijana kama 105 hivi, walituvamia kisha wakatuteka lakini wenzangu walifanikiwa kukimbia.

“Walinishika na kuanza kunibaka na walipoona nimezimia ndipo wakakimbia.

“Ukweli wameniachia majeraha na maumivu makali yasiyosimulika. Nawaomba watu wa haki za binadamu wanisaidie ili sheria itende hali yake kwa sababu huu ni unyanyasaji wa kijinsia,” alisimulia Pendo nje ya kituo cha polisi huku akitokwa machozi.

MKUU WA WILAYA ANENA

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Butiama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Annarose Nyamubhi alikiri kutokea kwa tukio hilo.

“Hilo tukio lipo lakini siwezi kulizungumzia zaidi kwa sababu lipo mikononi mwa polisi,” alisema Annarose.

KAMANDA WA POLISI

Gazeti hili lilipomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Rorya, ACP Philip Kalangi ili kuthibitisha tukio hilo alisema yupo nje ya mkoa ila atalifuatilia.

Leave A Reply