The House of Favourite Newspapers

Mgonjwa wa Kwanza wa Corona Afariki Tanzania

0

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto,  imethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vinavyotokana na corona — Covid-19 — nchini Tanzania kilichotokea alfajiri ya leo Machi 31, 2020, katika Kituo cha Matibabu cha Wagonjwa wa Corona kilichopo Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

 

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,  ambapo amesema mgonjwa huyo aliyepoteza maisha ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49.

“Nasikitika kutangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid -19 hapa nchini kilichotokea alfajiri ya leo tarehe Machi 31, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Mloganzila Dar es Salaam.

“Marehemu ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine, tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na tunatoa pole kwa ndugu hasa wa marehemu,” amesema Waziri Ummy.

Hadi sasa jumla ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19 nchini ni 19, aliyepona ni mmoja na aliyefariki dunia ni mmoja.

 

Leave A Reply