The House of Favourite Newspapers

Miaka 60 ya Uhuru Uwanja wa Uhuru

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amefanya kikao kazi Cha Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo amewaelekeza Viongozi Kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya na Mkoa kulibeba Jambo hilo.

 

RC Makalla amesema Maandalizi ya tukio Hilo la kihistoria yanakwenda vizuri na kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kueleza kuwa Mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha Hali ya Ulinzi na Usalama vinaimarishwa.

 

Aidha RC Makalla amesema katika kuelekea maadhimisho hayo kutakuwa na Matukio mbalimbali ikiwemo ziara za Viongozi kuzindua Miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Hata hivyo RC Makalla amesema tukio hilo litahudhuriwa na Viongozi wa mataifa mbalimbali wanaokuja kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Tanzania.

Leave A Reply