The House of Favourite Newspapers

Mabaki ya Kichwa cha Mwanafunzi Aliyeliwa na Mamba Yazikwa

0

BUCHOSA: Mabaki ya mwili wa mwanafunzi aliyekuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Nyakasasa iliyoko Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Thobias Mateso (11) yamepatikana na kizikwa kijijini kwako Nyakasasa.

Tukio la mwanafunzi huyo kuliwa mamba lilitokea jana Jumatano, Novemba 10, mwaka huu majira ya saa 11 za jioni wakati akioga katika Ziwa Victoria.

Ofisa Mtendaji Kata ya Nyakasasa, Judith Kitunde amethibitisha kupatikana kwa mabaki hayo leo Alhamisi, Novemba 11, ambapo kilipatikana kichwa pekee huku sehemu nyingine za mwili zikiwa zimeliwa, na baada ya hapo waliamua kufanya mazishi kijijini hapo.

Baba mzazi wa Marehemu, Mateso Kolontini amesema mwanae Thobias Mateso alikuwa mtoto wa 4 kwenye familia yake na ameacha pengo kubwa na masikitiko makubwa ndani ya familia yake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakasasa, Sebastian Masingine amesema tukio hilo ni la nne kutokea Kijiji hapo ndani ya mwaka mmoja na nusu. Amesema Kati ya matukio hayo matatu ni kujeruhi kwa waliwa na mamba na moja mtu kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba.

Mmoja wa wakazi Kijiji cha Nyakasaa, Prosikovia Lweikiza amesema uhaba wa maji kwenye kijiji hicho ndiyo chanzo kikubwa cha wananchi wa eneo hilo kuliwa na mamba wakati wakifanya shughuli zao mbalimbali kibinadamu katika Ziwa Victoria.

Leave A Reply