The House of Favourite Newspapers

Video: Miili Ya Askari Wanandoa Ilivyozikwa Kwa Heshima Mbeya, Risasi Zapigwa Angani…

0

MIILI ya wanandoa wawili, Sajenti Noah Simfukwe (30) na Agness Kiyeyeu (27) waliofariki kwa ajali siku tatu tu baada ya kufunga ndoa, imezikwa Makongorosi Chunya Mkoani Mbeya Desemba 23, 2022.

 

Wanandoa hao ambao walikuwa askari wa Jeshi la Polisi jijini Arusha, walifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Tanangozi, Iringa baada ya gari walilokuwa wakisafiria, Toyota Vitz lenye namba za usajili T164 DHH kugongana na basi Basi la Kampuni ya Luwinzo lenye namba za usajili T626BQE lililokuwa likitoka Ubaruku mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam. Walikuwa wakisafiri kutoka jijini Arusha kuelekea jijini Mbeya.

Leave A Reply