The House of Favourite Newspapers

Miili ya watu 34 yapatikana Bujumbura

0

151212112159_burundi_body__512x288_reutersMoja ya mwili ukiwa umefunikwa katika mji mkuu Bujumbura, Burundi.

Miili 34 imekutwa leo katika mji mkuu Bujumbura huku machafuko yakiendelea baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi tatu za jeshi.

Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.

Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni.

Machafuko yameendelea nchini Burundi tangu kutibuliwa kwa jaribio la kupindua serikali mwezi Mei na maandamano yaliyofanyika kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa mara nyingine.

Bw Nkurunziza alishinda uchaguzi uliofanyika Julai.

CHANZO: BBC SWAHILI

Leave A Reply