The House of Favourite Newspapers

Mil. 39 Zilizoyeyuka Kishirikina Zapatikana Laki 4 Kwenye ‘Kibubu’ – Video

FEDHA za kikundi cha kikoba cha kina mama cha Amani mkoani Arusha — Sh. milioni 39 — ambazo zinadaiwa kupotea kishirikina,  inasemekana ni Sh. 400,000 tu zimepatikana baada ya  mweka hazina wa kikundi hicho akiwa ameongozana na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuvunja sanduku lililokuwa linahifadhi fedha hizo na kukuta fedha hizo na nyaraka kadhaa tu.

 

Hilo limefanyika nyumbani kwa mtunza fedha wa kikundi hicho maeneo ya Ngusero, ambaye hawakufanikiwa kumkuta na akiwa ndiye mtuhumiwa wa kupotea kwa fedha hizo, aliyetajwa  kama Mama Abuu.

 

Mwanakikundi mmoja amesema miongoni mwa fedha ambazo zilizokuwepo ni ambazo zilibaki baada ya kutokea vurugu wakati wakisubiri kupatiwa fedha zao na kuambiwa zimepotea kishirikina.

 

Comments are closed.