The House of Favourite Newspapers

Mimi Mars: Najua Nina Shepu Mbaya

0

MUA, Ex, Shuga, Kodoo na nyinginezo kibao ni miongoni mwa ngoma kali kutoka kwa mwanadada mrembo Marianne Mdee au Mimi Mars ambaye amekuwa akifanya kazi chini ya Lebo ya Mdee Music inayomilikiwa na dada yake, Vanessa Mdee au Vee Money.

Gazeti la IJUMAA limefanya mahojiano maalum (exclusive) ambapo amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake, uhusiano wa kimapenzi na mengineyo.

IJUMAA: Tangu watu wameanza kukufahamu mpaka sasa umekuwa sio mtu wakuweka wazi uhusiano wako wa kimapenzi, sababu kubwa ni nini?

MIMI MARS: Hakuna sababu yoyote ya msingi ila nadhani ni mfumo tu ambao mimi mwenyewe nimejiwekea.

IJUMAA: Kwa mila za kiafrika ni nadra sana kuona mtoto wa kike anajitokeza hadharani na kusema ameshawahi kumtongoza mwanaume, vipi kwa upande wako hii hali imewahi kukutokea?

MIMI MARS: Ndiyo, ila ilikuwa kipindi nasoma lakini hivi ukubwani siwezi kuthubutu.

IJUMAA: Kwa nini unasema ukubwani huwezi kuthubutu?

MIMI MARS: Ok kwanza niwe mkweli sijawahi kukataliwa hivi ukubwani nikimfuata mwanaume nakumwabia nimempenda, lakini enzi za shule nilikuwa mtu wa ajabu.

IJUMAA: Na ulikuwa unamaanisha kuwatongoza au ilikuwa ni akili ya kitoto tu?

MIMI MARS: Awww! Shule nilikuwa namaanisha yani unakutana na hand some boy unaenda kumueleza hisia zako, na kipindi hicho nilikuwa sekondari, sasa kipindi hicho kidogo nilikuwa mnene kwa hiyo unaweza ukamfuata mwanaume halafu anakuzingua.

IJUMAA: Hebu tupe experience yakukataliwa ikoje?

MIMI MARS: (anacheka) Inauma, unaanza kuwaza kwani mimi nina kasoro gani, au niwe kama fl’ani, hapo unaanza kuangalia sasa wasichana ambao huwa anatoka nao, kwamba au uwe kama wale au labda uanze kuvaa kama wao, yaani unakuwa na maswali mengi kichwani.

IJUMAA: Ni kweli unatoka kimapenzi na msanii mwenzako Marioo?

MIMI MARS: No comment.

IJUMAA: Kwa nini unasema no comment?

MIMI MARS: Kwa sababu sipo kwenye mood yakuliongelea hilo.

IJUMAA: Wewe ni mtoto wa mwisho kwenu na mara nyingi watoto wa mwisho huwa wanadaiwa kuwa na vitabia fl’ani hivi vya usumbufu vipi kwa upande wako?

MIMI MARS: Ni kweli lakini binafsi siwezi kusema kama nilidekezwa wakati mdogo au niliachiwa huru, yaani kwa ufupi nilikuwa katikati, wazazi wetu walikuwa wakitusihi sana tuende kanisani, walikuwa wanatukataza kwenda hovyo kwa watu na vitu kama hivyo, mara nyingi maisha yetu yalikuwa ni ndani tu.

IJUMAA: Staa gani wa kike ndani na nje ya Bongo ambaye mapigo yake yanakuvutia sana?

MIMI MARS: Kwa nje navutiwa sana na Rihanna na kwa Bongo ni Nancy Sumari na Jackline Mengi.

IJUMAA: Vipi kuhusu mapigo ya Vanessa?

MIMI MARS: Vanessa anavaa vizuri sana na anapendeza, lakini kuna utofauti kwa sababu lazima uujue mwili wako pia unahitaji mavazi gani, kuna mavazi ya mtu mwenye mwili mkubwa na mtu mwenye mwili mdogo, mavazi yake yanaweza kuwa yananipendeza kumuangalia anavyovaa lakini sio mimi nivae.

IJUMAA: Umeshawahi kwenda kwa mganga kwa ajili ya kuboresha kazi zako unazozifanya?

MIMI MARS: Hapana.

IJUMAA: Hivi karibuni msanii wa Bongio Fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ aliweka wazi kuwa huwa anavaa vigodoro (shepu bandia) vipi kwa upande wako huwa unavivaa ili uwe na muonekano mzuri?

MIMI MARS: Mmmh! Hapana najua nina shepu mbaya yaki-Arusha lakini kigodoro ni kitu ambacho yani sijawahi hata kufikiria kwanza nitajihisi tofauti sana sitakuwa na amani, ila mkanda wa kubana tumbo sawa.

IJUMAA: Kwa unavyoona kuna dalili zozote za Vanessa kurudi kwenye gemu?

MIMI MARS: Nilishawahi kusema kwamba watu walimuelewa vibaya Vanessa hakusema anaacha muziki mazima bali alisema anapumzika kwa muda, hivyo nadhani bado yupo kwenye mapumziko akishamaliza watu wategemee kumuona tena.

IJUMAA: Unadhani ameacha pengo gani kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva?

MIMI MARS: Ametuachia pengo kubwa sana, kwa sababu katika wasichana wa Bongo Fleva ambao walikuwa wanaongoza kuipeperusha bendera ya Tanzania Vee alikuwa mmoja wapo, japo sasa hivi namuona Nandy, Zuchu na wao pia wanafanya poa sana.

IJUMAA: Kitu gani ambacho huwa unakikumbuka sana kwenye muziki wa Vanessa?

MIMI MARS: Mapigo yake bwana, yani ngoma alikuwa akitoa effort yake yote kufanya video, yani ukiambiwa Vanesaa Mdee anashusha ngoma ni ngoma kweli sio yakitoto, ni msanii ambaye alikuwa akitangaza kuachia ngoma unajua kabisa lazima itakuwa nzuri.

IJUMAA: Ulijisikiaje mara baada yakupewa tuzo ya muigizaji bora wa kike chaguo la watazamaji?

MIMI MARS: Kiukweli nilifurahi sana ilinipa moyo na inaendelea kunipa moyo kwamba kitu ninachokifanya kwa watanzania kinaonekana.

IJUMAA: Jambo la mwisho kwa mashabiki zako

MIMI MARS: Nawapenda sana na naomba wasichoke kunisapoti.

Makala: Memorise Richard, Bongo

Leave A Reply