The House of Favourite Newspapers

 Minu Aapa Kumuoa Snura!

0

MPENZI wa mwanamuziki wa Singeli nchini, Snura Mushi, Minhal Azad ‘Minu’ amesema kuwa, atakuwa mjinga aliyepitiliza kama hatamuoa mpenzi wake huyo kwa sababu ni mwanamke mwenye busara na anafaa kuwa mama wa familia yake.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Minu amesema kuwa, tangu ameanza uhusiano na Snura, ameweza kubadilisha sana maisha yake kutokana na uelewa mkubwa alionao, tofauti kabisa na uhusiano mwingine wowote aliowahi kupitia.

 

“Nitachekwa na kuonekana mjinga sana kama nisipofanya maamuzi sahihi ya kumuoa Snura, yaani kwangu ametosheleza kila kitu na busara zake kwangu, ndiyo msingi mkubwa sana. Yaani kifupi ni mwanamke wa kuoa,” alisema Minu.

STORI | Imelda Mtema, Risasi

Leave A Reply