The House of Favourite Newspapers

Misa ya Kuwaombea Marehemu Maria na Consolata Kabla ya Mazishi – Video

MIILI ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imefanyiwa ibada ya maombi na kuagwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) kabla ya kuzikwa katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo leo Jumatano, Juni 6, 2018.
Maria na Consolata ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa, watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.

Familia za baba na mama wa mapacha hao kutoka Tukuyu, Mbeya na Bukoba, Kagera, waliokuwa walezi wa mapacha hao, masista wa Consolata wa Iringa, na waombolezaji wengine,  wameungana katika kuwasindikiza mapacha hao katika safari yao ya mwisho duniani.

Comments are closed.