The House of Favourite Newspapers

Miss Czech Republic Krystyna Pyszková Ashinda Miss World

0
Miss Czech Republic, Krystyna Pyszková (24).

Miss Czech Republic, Krystyna Pyszková (24) ameshinda taji la 71 la shindano la urembo la dunia ‘Miss World 2023’ na kuwaongoza warembo wenzake 112 waliowania taji hilo.

Krystyna Pyszková amepokea taji hilo kutoka kwa aliyekuwa akilishikilia, Karolina Bielawska kutoka Poland.

Mshindi wa pili wa Miss World (1st runner-up) ni Yasmina Zaytoun kutoka Lebanon.

Mrembo wa Tanzania, Halima Kopwe, alifanikiwa kuingia 40 bora, nafasi ambayo katika mashindano hayo ilikuwa sawa na robo fainali.

Shindano hilo kubwa la urembo duniani kwa mwaka huu limefanyika katika ukumbi wa Jio World Convention Centre, katika Jiji la Mumbai, nchini India.

Warembo walioingia 12 bora na nchi zao kwenye mabano ni Kristen Wright (Australia), Maria Victoria Bayo (Jamhuri ya Dominican), Liza Gundowry (Mauritius), Paula Pérez (Hispania) na Lesego Chombo (Botswana).

Wengine ni Leticía Frota (Brazili), Krystyna Pyszková (Jamhuri ya Czech), Jessica Gagen (Uingereza), Sini Shetty (India), Yasmina Zaytoun (Lebanon), Aché Abrahams (Trinidad and Tobago) na Hannah Tumukunde wa Uganda.

Warembo walioingia nane bora ni Lesego Chombo (Botswana), Leticía Frota (Brazil), Krystyna Pyszková (Jamhuri ya Czech), Jessica Gagen (Uingereza), Sini Shetty (India), Yasmina Zaytoun (Lebanon), Aché Abrahams (Trinidad and Tobago) na Mganda Hannah Tumukunde.

Warembo walioingia nne bora ni Lesego Chombo (Botswana), Krystyna Pyszková (Jamhuri ya Czech), Yasmina Zaytoun (Lebanon) na Aché Abrahams wa Trinidad and Tobago.

Leave A Reply