MISS TANZANIA ALIVYOGUSWA NA HDIECA KUHUSU UTUNZAJI MAZINGIRA

Miss Tanzania, Elizabeth Makune akichangia mada kwenye kongamano la Mwanamke na Mazingira.

Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune  Jumamosi Feburuari 23  alikuwa mmoja wa waliohudhuria kongamano la Mwanamke na Mazingira lililoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya ya HDIECA inayojishughulisha na utunzaji wa mazingira.

Mgeni rasmi, Mjuni Chuchil (kulia) akikagua bidhaa za wajasiriamali waliopewa mafunzo na HDIECA.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa  Afisa Mazingira wa Mkoa Dar es Salaam, Mujuni Chachil ambaye naye ametangaza rasmi kujiunga na taasisi hiyo baada ya kubaini umuhimu wake.

 

Kongamano hilo lililoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HDIECA, Sara Pima  lilifanyika Makumbusho ya Taifa, Posta Jijini, na kuhudhuriwa na taasisi na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Dar ambapo walijadili changamoto zinazoyakabili mazingira.

Wahudhuriaji wakisikiliza kiumakini.

Wadau hao kutoka vikundi na taasisi mbalimbali waliafikiana kwa pamoja kulinda mazingira kwa kutoa elimu kwa wasio na elimu hiyo ili kuendelea kuishi kwenye dunia iliyo salama.

Mkurugenzi wa HDIECA, Sara Pima akitoa elimu ya mazingira.

Taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu ya mazingira sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni ambapo mpaka sasa imeshakuwa na malozi wa mazingira kwenye shule za msingi na sekondari ambao wanatoa elimu hiyo kwa wenzao.

 

Baada ya kongamano hilo Miss Tanzania aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi wanaposikia makongamano kama haya ili kupata elimu ambayo si rahisi kuipata bure kwa faida ya ulimwengu.

Mabalozi wa mazingira kutoka mashuleni wakiwa kwenye kongamano hilo.

Taasisi hiyo ambayo pia inahusika na masuala ya ujasirimali pia kwenye kongamano hilo wajasiriamali hao waliopata nafasi ya kuonesha ubunifu wa bidhaa zao na kuwauzia waliokuwa wakizihitaji.

Grayson Kavumo kutoka KIASI LTD ambaye ni mtaalamu wa mazingira akitoa elimu kwa wahudhuriaji.

 

PICHA/HABARI NA RICHARD BUKOS/GPL


Loading...

Toa comment