Mke wa R.O.M.A Amlipua Mbunge LIVE, Kisa ‘Zimbabwe’ (VIDEO)

Mama Ivan.

IKIWA ni siku moja tangu mkali wa michano na mwanaharakati wa kweli Rymes of Magic Attraction R.O.M.A kuachia video ya ngoma yake mpya aliyoipa jina la ‘Zimbabwe’, Nancy au Mama Ivan ambaye ni mke wa R.O.M.A amefunguka mengi kuhusu masahiri yaliyomo kwenye wimbo huo.

 

Akifanya mahojiano maalum kupitia kipindi cha Exclusive Interview cha Global TV, mama Ivan ameutaja msitari unaomuumiza na kumnyima usingizi ni kuhusu mmoja wa wabunge aliyetamka hadharani bungeni kuwa msanii huyo amemtukana Mkuu.

Msitari wenyewe;

 

..Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana Mkuu, atahukumiwa na mkono wa Mungu,…. kwanza lini na kwa nini? Mimi nimtukane Mjomba? Umepewa gari la wagonjwa mimi Tanga ananijengea bomba…!

 

“Huo ndiyo msitari ambao unaniumiza, nikikumbuka yule mbunge aliyesema muacheni atekwe, anamtukana Rais? Huyo mbunge hakufanya jambo zuri, kiukweli R.O.M.A hajawahi kumtukana Rais, ameimba kitu kilichomtokea, kilichomgusa na kipo moyoni. Sisi tumemwachia Mungu, tunasali sana na Mungu ndiye atahukumu mwisho wa siku,” alisema Mama Ivan.

 

Mama Ivan ameshukuru namna wimbo huo ulivyopokelewa na mashabiki wa R.O.M.A ambayo yamewashangaza wengi na kuvunja rekodi kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watanzania wote walioungana naye na kumfariji wakati wa matatizo.

MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment