The House of Favourite Newspapers

Mwakalebela Akiwa Rais Tu, Atafanya Haya

0
Frederick Mwakalebela.

KATIBU Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela anawania nafasi ya urais katika shirikisho hilo ambapo kipaumbele chake ni kuweka msingi wa utawala bora. Uchaguzi wa TFF unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St Gasper.

Mwakalebela ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa kipindi kirefu sasa TFF ilikosa misingi ya utawala bora ambayo ingeweka uwazi
katika mapato na matumizi ili kuvutia wadhamini.

Mwakalebela alisema: “Nikipata urais nitaanza na utawala bora kwa kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa.

“Nitaiangalia upya agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.

“Nitasimamia matakwa ya katiba ya TFF kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.”

NA: WILBERT MOLANDI| CHAMPIONI JUMAMOSI| DODOMA

Mwakyembe Ataja Vigezo kwa Uongozi Unaotakiwa TFF

 

Leave A Reply