The House of Favourite Newspapers

Mke Yamkuta Akitoka Kwenye Ngoma!

0
Sophia Mashala alivyoumizwa.

 

SOPHIA Mashala ( 29) mkazi wa Kijiji cha Kishapu wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga amekuwa katika mateso kwa miaka mitano sasa baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kutafunwa pua na fisi akiwa anatoka kwenye ngoma ya mtoto wa shemeji yake, iliyokuwa inafanyika katika Kitongoji cha Nyalusanga, kisha kunyofolewa pua ambapo sasa anadai kutelekezwa na mumewe.

 

Akizungumza na mwandishi wetu Jumapili iliyopita, Sophia alidai mumewe Solomon Ndilu amemtelekeza baada ya kukumbwa na janga hilo na sasa ameoa mwanamke mwingine, hivyo ameamua kudai talaka kwani tangu ashambuliwe na fisi mwaka 2011 mumewe hajawahi kumsaidia kwa lolote zaidi ya kuhudumiwa na wazazi wake.

 

Alisema hivi sasa anaishi kwa shida kwa sababu amekuwa akipumulia mdomoni na ameamua kudai talaka kutokana na mumewe kutomsaidia fedha za matibabu, hivyo akaamua kurudi nyumbani kwao ili akapate huduma za matibabu.

 

Sophia Mashala alivyoharibiwa

 

“Nimekuwa nikiishi nyumbani kwa wazazi wangu pamoja na watoto wangu wawili, baba yao katutelekeza, kinachosikitisha ni kwamba hata kuja kuwaona wanawe haji, sasa kwa kuwa ameoa mke mwingine nimeona bora nidai talaka yangu ili niwe huru,” alidai mwanamke huyo.

 

Alisema awali aliolewa na mume wake huyo kwa mahari ya ng’ombe 15, na kubahatika kupata watoto wawili, lakini baada ya kupata matatizo hayo wakwe zake walimtenga huku wakikataa kutoa pesa za matibabu hivyo kwa kusaidiwa na wazazi wake alizunguka katika hospitali mbalimbali nchini kutafuta tiba lakini bado anasumbuliwa na tatizo la kushindwa kupumulia pua.

 

Ndilu alipotafutwa na mwandishi wetu na kuulizwa kuhusu madai hayo mazito, alikiri kuoa mke mwingine lakini awali alikataa kutoa talaka kwa mwanamke huyo kwa kuwa bado anampenda.

 

Sophia Mashala akiwa ameketi

 

Alipobanwa na baba yake mzazi akiwa na mwenyekiti wa kijiji kuhusu tuhuma za kutomhudumia alisema tiba ya mkewe huyo inahitaji gharama kubwa na yeye hana uwezo.

Mwanamke huyo juzi alisema sasa atakwenda mahakamani kutafuta haki.

 

Sophia alipata masaibu hayo alipokuwa akitoka harusini pamoja na wenzake zaidi ya 30 Oktoba 16, 2011, majira ya saa 12 jioni, ghafla akavamiwa yeye tu kisha kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake huku mdomo na pua vikinyofolewa na mnyama huyo anayedaiwa kuwa wa kichawi.

Kwa yeyote aliyeguswa na habari ya mama huyu anaweza kumsaidia kwa kutumia namba yake 0768 718 846.

 

STORI: MWANDISHI WETU | UWAZI| KISHAPU

 

LIVE: Kijana Said Mrisho Aliyetobolewa Macho na Scropion Amtelekeza Mkewe

Leave A Reply