The House of Favourite Newspapers

Bashungwa Ampokea Mkongwe wa Filamu za Kihindi, Sunjay Dutt

0
Waziri Bashungwa (kushoto) akisalimiana na Sunjay Dutt muda mfupi baada ya msanii huyu kutua hapa nchini.

 

 

WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa amempokea hapa nchini msanii mkongwe wa filamu kutoka nchini India, Sunjay Dutt,  aliyekuja Bongo kwa lengo ni kudumisha muungano wa wasanii wa Bongo Muvi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Innocent Bashungwa alisema ugeni huo ni fursa kwa wasanii ili waweze kujifunza vitu mbalimbali kutoka kwa wasanii wa sehemu tofauti duniani.

Waziri Bashungwa na Sunjay Dutt wakiwa na wageni wengine waliofika kumpokea msanii huyo.

“Napenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya sanaa tumepata mgeni, dhamira ya Serikali kupitia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, lengo ni kudumisha muungano wetu kuelekea miaka sitini ya uhuru wa Tanzania.

 

“Kutakuwa na mkutano na wadau wa filamu tarehe 10 mwezi huu, pamoja na mgeni wetu Sunjay Dutt ili kujadili fursa za kushirikiana kati ya Tanzania na India katika sekta ya filamu hususani utayarishaji wa filamu bora zitazokuwa na ushindani wa soko ndani na nje ya nchi na pia awaambie safari yake kisanii pamoja na changamoyo zake alizopitia mpaka kuwa maarufu ili waweze kujifunza kutoka kwake.

Waziri Bashungwa akiongoza mkutano kwenye mapokezi ya mkongwe huyo wa filamu.

 

“Nashukuru nimekutana na muandaaji wa tuzo za kimataifa za filamu za WFF Word  Oscar Signature award Dkt.Fasi Khuram kwa ajili ya kupanga mipango ya awali ya maandalizi kwa kuwa tunatarajia kuwa wenyeji wa tuzo hizo mwaka 2023 zitafanyika  hapa Tanzania kwa hiyo tunaona kwamba serikali ya awamu ya sita imejipanga kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia Rais wetu.

 

“Kutakuwa na wasanii 50 kutoka nchi mbalimbali Duniani kwenye hiyo festival,  kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya mavazi,  michezo mbalimbali na mambo mengi ya sanaa na pia tutaonyesha utamaduni wetu kupitia wasanii wetu ili wageni watakaokuja waweze kujua tamaduni zetu.

 

” Na pia tunaangalia namna ya kufanya ili wasanii wetu waweze kwenda Dubai kujifunza vitu mbalimbali vya kisanii na kubadilishana mawazo, na kutangaza sanaa yetu na utalii, “alisema.

 

Nae Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt.Kiagho Kilonzo alisema kuwa wamefurahi kupata ugeni huo kwa kuwa imekuwa fursa kwa wasanii wa Tanzania kujifunza vitu kutoka kwake.

 

“Tumepokea vizuri ugeni wetu kutoka India hii ni hatua kubwa na jitihada za Serikali kufanya vitu vizuri kwa ajili ya sekta ya filamu nnchin itakuwa na muunganiko na India kwa hiyo tunatarajia wasanii wetu wanaendelea kutengeneza filamu bora zaidi,” alisema.

Leave A Reply