The House of Favourite Newspapers

Mkuki moyoni mwangu-54

0

DRACULA amefanikiwa kumchukua Catarina kutoka kwenye nyumba aliyofichwa na FBI akijifanya Padri aliyekuwa akienda kwenye nyumba hiyo kumpa Catarina msaada wa kiroho, akaaminika kama Padri Coronel Garsia!

Kwa ushirikiano na afisa wa FBI Clarence, aliyenunuliwa na Jackson Motown kwa fedha nyingi ili asaidie katika zoezi la kumuua Catarina, wamemchukua mpaka kwenye kilima kiitwacho New York Mountain Top ambako gari lake limegongwagongwa na katapila na baadaye kumchukua Catarina na kumlaza chini, Dracula amenyanyua nyundo juu kwa lengo la kumpiga nayo kichwani ili afe, baada ya hapo aingizwe kwenye gari lililogongwa na katapila ili ionekane ilikuwa ni ajali mbaya ya gari iliyomuua.Je, nini kitaendelea?SONGA NAYO…

CHUMBA kilikuwa na giza, haikuwa rahisi kugundua ilikuwa ni usiku au mchana, hewa pia ilikuwa nzito kwa sababu ya chumba hicho kukosa madirisha makubwa ya kutosha kuingiza hewa, mwanga uliokuwemo ulitoka kwenye mshumaa uliowaka pembeni mwa godoro lililotandikwa chini.

Juu ya godoro hilo alilala binadamu akiwa amefunikwa na shuka nyepesi ya rangi nyeupe, alionekana dhaifu kwa sababu ya aidha kuwa mgonjwa au mwili wake ulikuwa umepooza! Ghafla akajigeuza kuonyesha kuwa hakuwa amepooza, kichwa chake kikaangalia upande wa pili ambako aliketi mwanamke mzee mwenye umri kati ya miaka sitini na tano na sabini.

Alipojiangalia mkononi mwake, mwanaume huyo aligundua kulikuwa na sindano iliyomchoma mwilini na kuunganishwa na mpira mdogo mwembamba ulioelekea juu ambako chupa ya plastiki ilining’inizwa ukutani ikiwa imefungwa kwa bendeji nyeupe za hospitali, bibi kizee yule alitabasamu na kumfanya mwanaume aliyelala juu ya godoro pia afanye hivyo.

“Who are you?”(Wewe ni nani?) aliuliza aliyelala juu ya godoro.
“I am Mrs Thomas Edmund!”(Mke wa Thomas Edmund!)
“I can remember that name, Who is he?”(Ninalikumbuka jina hilo, ni nani huyo Thomas Edmund?)
“Your friend, the one who brought you here!”(Rafiki yako, aliyekuleta hapa!)

“And who am I? Do you know my name?”(Na mimi ni nani? Unalijua jina langu?)
“Yes!”(Ndiyo!)
“Tell me who am I, I have forgotten my own name!”(Niambie mimi ni nani, nimesahau jina langu mwenyewe!)
“Your name is Kevin!”(Jina lako ni Kevin!)
“Kevin? Where Am I from? And where Am I at the moment?”(Kevin? Ninatokea wapi? Na hapa nilipo ni wapi kwa sasa?)

“My husband told me, you are from Tanzania, East Africa, at the moment you are in New York!”(Mume wangu aliniambia unatokea Tanzania, kwa hivi sasa upo New York!)

“Yes! I can remember now! I came to New York looking for my fiencee, but someone wanted to kill me!”(Ndiyo! Nakumbuka sasa! Nilikuja hapa New York kumtafuta mchumba wangu lakini mtu mmoja anataka kuniua!)
“My husband told me the whole story, sorry for everything!”(Mume wangu aliniambia kila kilichotokea, pole kwa yote!)

“Where is he?” (Yuko wapi hivi sasa?)
“He will be here in a few minutes!” (Atakuwa hapa baada ya dakika chache!) aliongea mwanamke huyo akiendelea kutabasamu.

Muda mfupi baadaye mlango ulifunguliwa, akaingia mzee mwenye ndevu nyingi ambaye baada ya macho ya Kevin kutua tu usoni kwake alimtambua, ndiye aliyemkuta kwenye shamba la maua akijaribu kujiokoa kutoka mikononi mwa Jackson Motown aliyetaka kumuua.

“You are back from hell?” (Umerejea kutoka Kuzimu?) aliuliza mzee huyo akicheka.
“Yes, sure!” (Ndiyo, hakika!)
“Everybody knows you are dead!” (Kila mtu anajua wewe ni marehemu!)
“Really?” (Kweli?)
“Yes!” (Ndiyo!)

“What happened?” (Kilitokea nini?)
“It is a long story, but I attended your funeral in Dar es Salaam at the Kinondoni Cemetry!” (Ni habari ndefu, lakini nilihudhuria mazishi yako jijini Dar es Salaam kwenye Makaburi ya Kinondoni!)
“Oh my God! You have been to Dar es Salaam?” (Oh Mungu wangu! Umeshafika Dar es Salaam?)
“I went there for your funeral!”(Nilikwenda kule kwa ajili ya mazishi yako!)

“Please tell me the whole story!” (Tafadhali nieleze kisa kizima!)
“They wanted you dead so I gave them what they needed!” (Walitaka ufe n kawapa walichokihitaji!)
Mzee Thomas Edmund aliketi vizuri kitini na kuanza kumsimulia Kevin kilichotokea mpaka akawa hai muda huo wakati dunia nzima ilikuwa ikielewa alishakufa na kuzikwa, Kevin alibaki kimya akimsikiliza jinsi alivyoanza siku aliyokutana naye na kumsimulia yote yaliyompata, mzee Thomas Edmund akakiri kumwonea huruma na moyoni mwake kupanga kumwokoa kwa sababu yeye pia alikuwa miongoni mwa waliochukia udhalimu wa Jackson Motown.

“In my farm house I lived with my dogs but my wife who is a retired Physician, lived here in New York, so when I planed your rescue I had to think of how to fake your death, do you remember the day I left you for downtown?”(Kwenye nyumba yangu ya shambani niliishi na mbwa wangu tu lakini mke wangu ambaye ni daktari mstaafu aliishi hapa New York, nilipopanga kukuokoa ilibidi nifikirie jinsi ya kutengeneza kifo chako cha uongo, unakumbuka ile siku niliyokuacha nikaja mjini?)

“Yes I do!”(Ndiyo naikumbuka!)
“I am a retired Marine, I came here to get a bomb from a friend of mine who work at the New York Arsenal!” (Mimi ni mwanajeshi mstaafu, nilikuja hapa kufuata bomu kutoka kwa rafiki yangu anayefanya kazi kwenye ghala la silaha la New York!)

“Go ahead!” (Endelea!)
“When I came back to the farm house, I had a dead body I got from New York hospital and bought sleeping pills from CVS Pharmacy too.

You drank the pills in a cup of milk without knowing, few minutes later you fell asleep, all I deed was to carry you into my car and placed the dead body in the house, then planted the bomb to explode five hours later, I wanted everyone to know you exploded in that house!” (Niliporejea kwenye nyumba ya shambani nilikuwa na maiti niliyoipata hospitali ya New York na pia nilikuwa nimenunua vidonge vya usingizi kutoka Duka la Dawa la CVS, ulivinywa vidonge hivyo kwenye maziwa bila kufahamu, muda mfupi baadaye ulisinzia, nilichokifanya ni kukubeba na kukupakia ndani ya gari kisha nikaweka maiti ndani ya nyumba, baada ya hapo nikatega bomu lilipuke saa tano baadaye, nilitaka kila mtu ajue umefia ndani ya nyumba ile!) aliongea mzee Thomas Edmund, jambo moja ambalo hakulifahamu ni kwamba Kundi la Jackson Motown nalo lilikuwa limepanga mpango huohuo, mabomu mawili yalitegwa ndani ya nyumba moja, lilipolipuka moja likalipua na lingine, Jackson Motown akajisikia mshindi alipopewa taarifa ya kufa kwa Kevin ndani ya nyumba hiyo, vivyo hivyo Thomas Edmund akajisikia bingwa kwa kuudanganya ulimwengu.
Kevin alipelekwa moja kwa moja nyumbani kwa Thomas Edmund katikati ya Jiji la New York, akafichwa kwenye chumba kilichokuwa chini ya jengo refu ambalo familia ya Thomas Edmund ilipanga nyumba moja ya chini. Kilikuwa chumba kidogo chenye hewa nzito, alichowekewa ni godoro tu sakafuni, wazee hao wawili wakakubaliana kumtunza kwa siri mpaka hali itakapotulia ndipo wamtafutie namna ya kuondoka Marekani kurejea Tanzania bila mtu yeyote kugundua.

Ingawa alikuwa na siri hiyo moyoni mwake, mzee Thomas Edmund aliamua kuhudhuria mazishi ya mtu ambaye hakuwa Kevin, yote hiyo ikiwa ni kuudanganya ulimwengu na kufanya iwe vigumu kwa mtu yeyote kudhani Kevin alikuwa hai, alimhurumia sana Catarina alivyokuwa akilia msibani, moyoni alitamani amsogelee na kumwambia “mchumba wako yuko hai” lakini alishindwa kufanya hivyo akihofia usalama wa Kevin.

“So that’s what happened! We have been sedating you ever since you came here, that’s why you have no memory!” (Kwa hiyo hayo ndiyo yaliyotokea! Tumekuwa tukikupa dawa ya usingizi tangu ufike hapa, ndiyo maana kumbukumbu zako ni mbovu!)

“Thank you so much Mr and Mrs Edmund

”(Ahsanteni sana bwana na bibi Edmund!)
“My wife has been feeding you intravenously!”(Mke wangu amekuwa akikulisha kwa njia ya mshipa!)
“Thank you mom!”(Ahsante mama!)

“You are welcome, I am just happy that you are alive!”(Karibu, ninafurahi tu kwamba uko hai!)
“And where is Catarina?”(Na Catarina yuko wapi?) Kevin aliuliza, bwana na bibi Edmund wakaangaliana, hawakuwa na jibu la kumpatia.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Ijumaa katika Gazeti la Championi Ijumaa.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply