The House of Favourite Newspapers

Mkuu Wa Kampeni Za Donald Trump Ahukumiwa Kwenda Jela

 

MENEJA wa zamani wa kampeni za Rais wa Marekani, Donald Trump, aitwaye Paul Manafort,  amehukumiwa kifungo cha miezi 47 jela kwa udanganyifu katika ulipaji wa kodi na benki.

 

Alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuficha mamilioni ya Dola wakati alipokuwa balozi nchini Ukraine. Anatarajiwa kuhukumiwa katika kesi nyingine wiki ijayo kwa kufanya kampeni kinyume cha sheria.

 

Mashtaka hayo yalitokana na na uchunguzi uliofanyika akiwa mmoja wa maofisa wa kampeni ya Trump ambao walifanya njama na Urusi ili kumwezesha apate ushindi katika uchaguzi wa 2016.

 

Balozi maalumu wa wizara ya sheria ya Marekani, Robert Mueller, anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake wa miezi 22 ambao unalenga dhidi ya urais wa Trump.

Comments are closed.