The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Majeshi Kenya Afariki Kwa Ajali ya Helikopta

0

Rais William Ruto wa Kenya amethibitisha taarifa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (CDF) Francis Ogolla amefariki dunia kwa ajali ya helikopta.

Ruto amesema Jenerali Ogolla alifariki Alhamisi mchana baada ya helikopta ya Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF) kupata ajali huko Sindar, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet.

“Ninahuzunika sana kutangaza kifo cha Jenerali Francis Omondi Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.

Rais Ruto alisema pamoja na Jenerali Ogolla katika ajali walikuwepo maafisa wengine 11 wa kijeshi, tisa kati yao walifariki pia huku wawili wakipona.

Maafisa wengine waliokufa katika ajali hiyo ni Brigedia Swale Saidi, Kanali Duncan Keittany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu, Nahodha Sora Mohamed, Nahodha Hillary Litali, Sajenti Mkuu John Kinyua Mureithi, Sajenti Cliphonce Omondi, na Sajenti Rose Nyawira.

Leave A Reply