The House of Favourite Newspapers

Mkwasa: Simba Wanafungika Mbona

0

IKIWA kesho Alhamisi Simba watashuka dimbani kucheza dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kocha wa Ruvu, Charles Mkwasa amesema kuwa Simba ni bora lakini wanafungika.

 

Mkwasa alisema hakuna timu ambayo haifungwi kwa sababu soka ni mchezo wa makosa na yeye anajua kuwa Simba wana udhaifu mahali na kama vijana wake watafuata maelekezo wanakwenda kushinda mchezo huo.

Akizungumza na Championi Jumatano Mkwasa alisema: “Simba ni timu bora sana kwa sasa, wachezaji wake wanajiamini mno, lakini bado kuna mahali wana udhaifu na kama ukifanyia kazi unawafunga.

 

“Mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu Simba, lakini kila timu inafungika na mimi naujua udhaifu wa Simba ambao siwezi kukuambia hapa. Wacha tusubiri siku ya mechi tuone itakavyokuwa.”

STORI: ISSA LIPONDADar es Salaam

Leave A Reply