The House of Favourite Newspapers

Mlima Kenya Wawashwa Moto Na Walima Bangi

 

MOTO unaodaiwa kuwashwa na wakulima wanaotaka kupanda bangi unatishia maelfu ya hekari za misitu ya mianzi katika Mlima Kenya au Mount Kenya. Tayari moto huo umeharibu kilomita 80 mraba za ardhi yenye nyasi na sasa unatishia misitu ya jadi.

 

Misitu mikubwa ya mianzi inapatikana katika eneo la Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa shirika la utafiti wa kimataifa wa ukulima (CGIAR) ni sawa na takriban asilimia 3 hadi 4 za misitu jumla ya mianzi au ‘bamboo’ kama inavyojulikana.

 

Moto huo ulioanza siku saba zilizopita, unateketeza  maeneo mawili na umekuwa ukisambaa kutokana na upepo na joto kali.

 

Shirika la Wanyama Pori limeeleza kwamba limekuwa likiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo na kwamba maofisa wa zimamoto wamepiga kambi katika eneo hilo wakiendelea na jitihada za kuuzima.

 

Watu wa  eneo hilo wamekuwa wakisaidiana na maofisa wa misitu na mashirika ya kibinafsi ya kuhifadhi mazingira, ambao wana rasilmali za msingi kukabiliana na ukubwa wa moto huo. Wakulima wanatuhumiwa kuuwasha moto huo wakijaribu kulisafisha eneo la kuwawezesha kupanda bangi na sasa moto huo unatishia mojawapo ya maeneo matano ya juu yanayofahamika kama “water towers”, ambako ni chanzo cha maji kwa mito kadhaa na chanzo cha robo-tatu ya maji yanayosambazwa nchini.

 

Moto huo, katika eneo jingine,  unatishia misitu ya mianzi yenye ukubwa wa hekari 40,000.

Mount Kenya ni mlima wa pili kwa urefu barani Afrika.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.