The House of Favourite Newspapers

Mlinzi Aliyemwamuru Waziri Kupanga Foleni Afukuzwa Kazi

0

MAHAKAMA nchini Kenya imehalalisha aliyekuwa mlinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Daizy Cherogony, kufukuzwa kazi kutokana na kumtaka aliyekuwa Waziri wa Elimu, Dkt. Fred Matiang’i,  kukaa kwenye foleni akaguliwe. Cherogory alifungua kesi baada ya kufukuzwa  2017.

 

Mahakama imetoa uamuzi huo na kusema kwamba kitendo cha dhihaka alichofanya  Cherogony dhidi ya  Matiang’i kinatosha kwa mwajiri wake, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KAA), kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.

 

Cherogony alifungua kesi dhidi ya KAA kwa madai kuwa kitendo cha yeye kufukuzwa kazi hakikufuata sheria, na pia alidhalilishwa na mwajiri huyo na kutaka alipwe fidia KSh milioni 2.4 (TSh milioni 55).

 

Amesema katika siku ya tukio, Aprili 5, 2017 abiria uwanjani hapo walikuwa wakipiga kelele, na alipomuona Waziri Matiang’i alimtaka apange foleni kwa ajili ya ukaguzi, na kwamba kitendo hicho hakikukiuka sheria wala taratibu yoyote ya KAA.

Leave A Reply