The House of Favourite Newspapers

Mnyama alivyoliwa Taifa mchana kweupeee

0

IMG_7999
Kiungo wa Simba, Awadhi Juma akimiliki mpira.

Said Ally na Ibrahim Mussa
MBIO za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa timu ya Simba zimepata ugumu baada ya timu hiyo kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa jana jijini Dar.

Simba ambayo kama ingeshinda ilikuwa irejee kileleni katika msimamo wa ligi hiyo, sasa imebaki na pointi 57 katika michezo 25 wakati Yanga imebaki kileleni ikiwa na pointi 59 katika michezo 24.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi ndogo, ilishuhudiwa bao hilo pekee likifungwa na Wazir Junior katika dakika ya 20, kitendo kilichofanya shabiki mmoja wa Yanga kumzawadia mchezaji huyo shilingi 70,000 ikiwa ni ishara ya kuonyesha kufurahishwa na mchezaji huyo kufunga bao hilo.

Shabiki huyo ambaye jina lake halikufahamika, alimuita Wazir wakati akitoka na kumhesabia noti saba za shilingi 10,000 kisha kumkabidhi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya.

IMG_7984Toto imefikisha pointi 30 katika michezo 27, hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kukwepa kushuka daraja.
Simba ambayo katika mchezo huo ilimpoteza beki wake wa kulia, Hassan Kessy katika dakika ya 47 kutokana na kumchezea vibaya straika wa Toto, Christopher Edward kisha kupewa kadi nyekundu, ilionyesha kutokuwa na makali hasa kipindi cha pili, lakini hata baada ya kubadilika na kucheza soka la kasi bado ilishindwa kuipenya ngome ya Toto.

Kocha wa Simba, Jackson Mayanja aliondolewa uwanjani na mwamuzi kutokana na kilichoonekana kumtolea lugha kali mwamuzi wa kati, Ahmada Simba kisha kocha wa makipa wa Simba, Adam Abdallah kuchukua majukumu ya kuiongoza timu.
Baada ya mchezohuo, Adam alisema kupoteza mchezo ni jambo la kawaida, wanajipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata lakini bado wapo kwenye mbio za ubingwa.

IMG_8050….Wachezaji wa Toto wakishangilia ushindi huo.

Kocha wa Toto, John Tegete alisema: “Nawapongeza wachezaji wangu kwa kuwa wamefanya kile nilichowaelekeza kufanya, walitumia nguvu kwa kuwa najua wachezaji wa Simba wengi hawana nguvu kama walivyo wangu.”
Aidha, baada ya mchezo huo, mashabiki wa Toto na wale wanaodhaniwa kuwa na Yanga, walikuwa wakishangilia na kulisukuma basi la Toto, hali iliyosababisha polisi kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya, zoezi ambalo lilifanikiwa.

Pia wachezaji wengi wa Simba walitoka uwanjani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali kutokana na kuonekana kuwa mashabiki wao wengi walikuwa na hasira nao.

Leave A Reply